t

Update

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Inclusive Development for Citizens platform and services:


Wanasiasa wanaweza kuwa daraja zuri au baya katika elimu.

Wanasiasa wanaweza kuwa daraja zuri au baya katika elimu.

 

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 11 (2) “Kila mtu ana haki ya kujielimisha, na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.”

Katiba imetoa haki ya kupata elimu na kupata huduma za kijamii bila ubaguzi wa aina yoyote ile, Watoto wa kike nchini wamekuwa na changamoto ya kubaguliwa kupata elimu pale wanapopata ujauzito, Tanzania imekuwa ikitumia sheria nyingine kuondoa watoto wa kike mashuleni kitu ambacho ni kinyume na takwa la katiba yetu, hakuna sheria inayotakiwa kutugwa hali inapingana na sheria mama yaani katiba ya nchi.

Hivyo basi kwa kuzingatia matakwa ya katiba Wanafunzi wanapaswa kupata elimu pasipo vikwazo vya aina yoyote, Elimu haipaswi kutengwa wala kuwekwa mbali na mtoto bali vyombo vya maamuzi vinapaswa kumrahisishia mtoto kupata elimu stahiki kulingana na mahitaji ya jamii kwenye ukweli kwamba hakuna maendeleo katika jamii pasipo mtoto kupata elimu.

Mwongozo wa elimu wa mwaka 2009 http://idc-tz.org/news/guidelines-on-how-to-enable-pregnant-school-girls-to-continue-with-their-studies-1

Ulitoa utaratibu wa mwanafunzi aliyepata ujauzito kuendelea na masomo lakini Mwongozo huu haukupitishwa na serikali  katika utekelezaji wake, kwahiyo hautumiki na Haki ya elimu katika katiba haija aininshwa katika haki za msingi za binadamu hivyo kutokana na hali hii inapelekea mazingira magumu na kuweka giza la jinsi gani mwanafunzi aliyepata ujauzito anarudi shule kwa namna gani.

 

Serikali inapaswa itambue wanafunzi wanakumbana na changamoto nyingi ambazo huwapeleekea kupata ujauzito hivyo basi inatakiwa iweke mwongozo mzuri  ambao utatoa dira ni kwa namna gani mwanafunzi aliyepata ujauzito atarudi shule lakini pia haki ya elimu iingizwe katika haki za msingi za binadamu ili utekelezaji wake uwe wa lazima hii itasaidia wanafunzi kupata ulinzi na uhakika wa kupata elimu bila vikwazo. Wanasiasa wanapaswa kuelewa kwamba jamii bora inatengenezwa na maarifa na hekima yatokanayo na elimu. Kwahiyo wanatakiwa kuihimiza serikali kutengeneza sheria na mwongozo wa elimu utakaotoa fursa kwa mtoto wa kike aliyepata ujauzito kurudi shule, Kama haitoshi wanasiasa wanapaswa kupeleka miswada binafsi bungeni.

 

MWISHO NA MUHIMU: Suala tete la mwanafunzi kupata ujauzito linasababishwa na sababu nyingi zikiwemo matatio yaliyokita mizizi katika familia nyingi hususani umasikini, uvunjifu wa maadili unaosababishwa kwa kiasi kikubwa na ukuaji wa sayansi ya teknolojia, kukua kwa makundi ya vijana wanaojihusisha na makundi haramu ya madawa ya kulevya na kuongezeka kwa wimbi la ubakaji nchini. Hivyo basi jamii inapaswa kupewa elimu ya ziada kuhusiana na umuhimu wa mtoto wa kike kupata elimu katika jamii, Pia serikali inapaswa kutengeneza sera na sheria zenye kutoa ramani ya jinsi gani mtoto aliyepata ujauzito anarudi shule.

Kuna wanafunzi wamepata mimba kwa kubakwa

 #ArudiShule #ElimuBilaUbaguzi #ActiveCitizens


download REPORT Posted on : 07 June, 2022