t

Update

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Inclusive Development for Citizens platform and services:


MFUMO KANDAMIZI KWA MTOTO WA KIKE

Wanafunzi wasichana wa Kitanzania wanakabiliwa na vikwazo vingi kupata elimu ikiwemo mazingira duni ya kujifunzia, hali duni ya kiuchumi kwa baadhi ya familia, kutozingatiwa kwa mahitaji maalumu ya watoto wa kike, unyanyasaji wa kijinsia , kukosa elimu ya afya ya uzazi au makuzi na umbali mrefu kati ya makazi na shule na hii inatokana na umasikini mkubwa katika jamii nyingi za kiafrika.

 

Kuna juhudi kubwa ya kusaidia wanawake kupata elimu lakini hii inafanyika zaidi katika ngazi za juu za elimu, wasichana kupewa nafasi maalum na kadharika, lakini kwenye msingi wa elimu kuna changamoto nyingi sana zinazohitaji jamii na serikali kupambana ili kuziondoa.

 

Moja ya changamoto kubwa sana kwa watoto wa kike wanapokuwa katika umri wa mdogo na wa kubalehe wanakosa elimu ya mimba za utotoni na kunyanyashwa kijinsi. Ni vyema kama jamii tuchukue hatua ya kuboresha mazingira ya shule ya watoto wa kike wasome kwa usalama, lakini pia kuwa na ulazima wa kulinda watoto wa kike katika jamii dhidi ya makundi mbalimbali yanayojiusisha na vitendo vya ngono na vijana wa kike wakiwa mashuleni.

 

Ili kudhibiti mimba zisizotarajiwa kwa watoto wetu wanapokuwa mashuleni hatua ya kwanza ni kutoa elimu ya afya ya uzazi au makuzi, watoto waelezwe na kuelimishwa kuhusu miili yao na kujulishwa athari za kushiriki vitendo vya ngono wakiwa na umri mdogo, lakini pia waelezwa changamoto wanazoweza kupata kama vile ujauzito katika umri mdogo ambao unaweza ondoa kabisa ndogo zao kupata elimu.

 

Wanaharakati nchini wanapashwa kushikamana kwa pamoja na kupigania mfumo bora wa kurusisha watoto wa kike shule pale wanapopata ujauzito,wanapashwa kushikamana kwa pamoja na kupigania mfumo bora wa kurudisha watoto wa kike shule pale wanapopata ujauzito, Kwa sasa tuna mfumo huu kandamizi kwa haki za wanafunzi hususani wa jinsia ya kike ni lazima ubadilike ili kuweka usawa kwa watoto wote, Kama wanaharakati watasimama imara dhidi ya mfumo huu kandanimizi na baguzi kwa haraka utaondolewa na serikali. Wanaharakati wana nafasi ya kuchochea haki nchini lakini pia kwa nafasi yao wanatakiwa kuhimiza usawa ili kuchochea kwa kasi serikali kubadili mfumo, ili kuwasadia wanafunzi wa kike waondokane na mifumo hiyo ambayo inanyima haki zao.

 

Ni wajibu wa serikali na jamii kutafiti na kupigania mazingira bora. Mazingira bora ya shule na katika jamii ndio mwarobaini wa changamoto ya ujauzito wa watoto wa kike katika umri mdogo. Kuwe na sheria bora na takwimu kuhusu watoto wanaoshindwa kuendelea na masomo ili tuweze tafuta vyanzo vya tatizo hili. Ushirikiano wa jamii na serikali unaweza kuondoa tatizo la ujauzito kwa watoto wa shule kwa haraka na hakika zaidi.

 

 

Tunapowakataza watoto wa kike wasiendelee na masomo pindi wanapopata ujauzito wakiwa shuleni, asilimia kubwa ya watoto wanaopata changamnoto ni  watoto wa masikini ambao watashindwa kwenda katika shule binafsi, maana tegemeo lao ni shule za umma. Hivyo utaratibu wa kuzuia watoto waliopata mimba kuendelea na masomo katika shule za umma  unaweka tabaka kubwa sana katika jamii. Watoto waliotoka katika familia zenye kipato huwa na uhakika na elimu kuliko waliotoka katika familia zisizo na kipato, hii ni adhabu ambayo inaondoa na kuua kabisa malengo ya maendeleo kwa watoto hawa..

 

Mwongozo wa Mwaka 2009  http://idc-tz.org/news/guidelines-on-how-to-enable-pregnant-school-girls-to-continue-with-their-studies-1 unatoa fursa kwa mtoto wa kike kufanya mtihani wa taifa endapo atabainika kuwa atakuwa na ujazitoka katika kipindi cha mtihani. Serikali ione haja sasa ya kuurudia mwongozo huu unaotoa fursa  kwa mtoto wa kike kurudi shule akijifungua kama walivyofanya Tanzania bara Mwaka 2010. Ambapo  Zanzibar walifanikiwa kutunga sheria ya kumlinda mtoto wa kike sheria inayotoa fursa kwa mtoto wa kike kurejea shuleni na kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

Tunatoa wito kwa Umoja na mshikamano  kwa Watanzania wote kuungana pamoja na kupinga mfumo wa kibaguzi katika utoaji wa elimu, serikali ikae na wadau wa elimu na kuondoa vikwazo hivi vyote katika utoaji wa elimu.

#ArudiShule #ElimuBilaUbaguzi


download REPORT Posted on : 09 June, 2022